News

Watu 4 waaga dunia wakati wa Sabasaba

Published

on

Watu wanne wamethibitishwa kuaga dunia wakati wa maandamano ya kuadhimisha miaka 35 ya kumbukumbu za Sabasaba ambapo watu 2 wamepiga risasi na kufariki katika maeneo ya Kitengela, wawili katika maeneo ya Kangemi na mtu mmoja katika maeneo ya Olkalou.

Kamanda wa Polisi kaunti ya Nyandarua Stellah Cherono alithibitisha kupigwa risasi kwa mkaazi wa Olkalou kaunti ya Nyandarua, akisema mtu huyo alipigwa risasi na kufariki wakati wa makabiliano kati ya maafisa wa polisi na waandamanaji.

Cherono aliwaonya vijana dhidi ya kuwashambulia maafisa wa polisi, akisema jukumu la maafisa wa polisi ni kuhakikisha usalama unaimarishwa lakini vijana wamekosa busara na kushambulia maafisa wa polisi kwa mawe.

Tayari mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yameikosoa serikali kwa kuendelea kushuhudiwa kwa maafa ya kila wakati wa maandamano, wakisema serikali ni lazima iheshimu katiba ya nchi ambayo inaruhusu maandamano ya amani.

Hata hivyo baada ya wakenya waliyojeruhiwa vibaya wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali mbalimbali huku Shirika la Msalaba Mwekundi nchini likisema idadi ya wale waliojeruhiwa inazidi kuongezeka.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version