News

DCI yaruhusiwa kufukua makaburi Kwa Binzaro Kilifi

Published

on

Idara ya upelelezi wa jinai DCI imepewa ruhusa na mahakama ya Malindi, kuanza kufukua makaburi yaliyotambuliwa katika kijiji cha Kwa Bi Nzaro kilomita sita kutoka eneo la Shakahola eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.

Hii ni baada ya makaburi zaidi kugunduliwa katika eneo hilo lenye msitu na  kuzua taharuki miongoni mwa wakaazi, huku ikihofiwa kuwa huenda wafuasi zaidi wa dhehebu potovu katika eneo hilo wamefariki.

Wizara ya usalama nchini ilisema imetibua kuenea kwa dhehebu hilo ambalo linakisiwa kuandamana na mafunzo ya itikadi kali kama ilivyoshuhudiwa katika msitu wa Shakahola miaka miwili iliyopita.

Oparesheni ya polisi ilifichua boma lililoko kwenye ardhi ya ekari tano linaloaminika kutumika kuwahifadhi wafuasia wa dhehebu potovu.

Wakaazi katika kijiji hicho walihofia huenda kunamiili mingine ambayo imezikwa katika sehemu hiyo ya ardhi baada ya mwili na mafuvu ya kichwa kupatikana maeneo hayo.

Mshukiwa mkuu anayedaiwa kuendeleza imani hio ni jamaa mmoja aliyeokolewa kutoka Shakahola nakurejeshwa kwa familia yake kaunti ya Siaya kabla ya kurejea Kilifi mapema mwaka wa 2025.

Alikamatwa pamoja na wengine na kufunguliwa mashtaka mahakamani Malindi kaunti ya Kilifi.

Taarifa ya Joseph Jira. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version