Sports

Winga Wa Colombia Luis Diaz Sasa Ni Mali Ya Bayern

Published

on

Klabu ya Bayern Munich, inayoshiriki Ligi Kuu ya Bundesliga nchini Ujerumani, imetangaza kumsajili winga wa Colombia, Luis Díaz.

Hatua hii imekuja baada ya Bayern Munich na Liverpool kufikia makubaliano kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo kwa ada ya pauni milioni 65.5.

Díaz, mwenye umri wa miaka 28, aliwasili mjini Munich hapo jana kwa ajili ya vipimo vya kitabibu kabla ya kutia saini mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa Ujerumani.

Mchezaji huyo alijiunga na Liverpool mwaka 2022 akitokea klabu ya Porto kwa ada ya pauni milioni 37. Tangu wakati huo, ameifungia Liverpool mabao 41 katika mechi 142 alizocheza uwanjani Anfield.

Nyota huyo aliondoka kwenye kambi ya mazoezi ya Liverpool mjini Hong Kong hapo jana na kujiunga rasmi na waajiri wake wapya kwa maandalizi ya msimu mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version