National News
Gavana Mung’aro Aagizwa Kulifanyia Marekebisho Baraza Lake la Mawaziri
Baadhi ya wakaazi kaunti ya Kilifi wamemtaka gavana wa kaunti hiyo Gedion Mung’aro kulifanyia marekebisho baraza lake la mawaziri kwa madai ya kufeli kutekeleza wajibu wake kikamilifu.
Kulingana na Mwakilishi wa vijana wadi ya Mtepeni kaunti hiyo Wisdom Ndoro, baadhi ya mawaziri hawafahamu wa majukumu yao ya kikazi licha ya kupewa raslimali za kutosha kwa lengo la kufaidisha wakaazi.
Ndoro amemuonya Gavana Mung’aro kuwa wananchi wa Kilifi watathimini utendakazi wake kabla ya kufanya maamuzi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2027
Ndoro amesema Gavana Mung’aro ameshindwa kutatua suala la uskwota licha ya kuwa na uwezo wa kusaidia wakaazi kutatua tatizo hilo.
Wakati huo huo amesema suala la ukosefu wa maji safi katika kaunti ya Kilifi linaendelea kutatiza wakaazi, akidokeza kwamba maeneo ambayo Gavana alizindua miradi ya maji hivi karibuni kufikia sasa hakuna maji yanayowafikia wakaazi.