News
Mapato ya Wavuvi hapa Kilifi yameongezeka
Mwenyekiti wa muungano wa wahudumu wa maboti kaunti ya Kilifi Shallo Issa maarufu captain Shallo amesema kuwa mapato ya wavuvi msimu huu yameongezeka ikilinganishwa na hapo awali.
Katika mazungumzo ya kipekee yaCoco fm, captain Shallo amesema kuwa wavuvi wote wanaotumia vifaa vya hali ya juu sawa na wale wavuvi wadogowadogo wameimarika kimapato muda huu.
Shallo amesema kuwa wavuvi hao wamekuwa wakiuza samaki kwa wingi sio tu hapa Kilifi lakini pia kwenye kaunti nyinginezo za Kenya sawa na taifa jirani la Tanzania.
Wakati huohuo Shallo amedokeza kuwa rais William Ruto kupitia wizara ya uchumi na raslimali za baharini na maziwa, analenga kuweka sehemu tatu ambazo zitajengwa bandari ndogo katika kaunti hii ya Kilifi.