News
Bunge la kitaifa kuwahoji makamisha wa IEBC
Bunge la kitaifa, Jumamosi, Mei 31 linatarajiwa kuanza kuwapiga msasa mwenyekiti na makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
Ni shughuli iliyoratibiwa kufanyika katika majengo ya bunge na ambayo inajiri siku moja tu baada ya mahakama kuu nchini kuliagiza bunge la kitaifa kutimiza wajibu wake kikatiba la kuwapiga msasa makamishna hao kabla ya kuapishwa .
Mnamo Alhamisi Mei 29, katika mahakama kuu ya Milimani jijini Nairobi ,Jaji Lawrence Mugambi alitoa uamuzi wa kusitisha shughuli za kuapishwa au kuchapsiwa katika gazeti rasmi la serikali majina ya Makamishna hao kabla ya kupigwa msasa na bunge la taifa.
Rais William Samoei Ruto, mnamo Mei 9, 2025, aliwasilisha majina saba ya makamishna wateule 6, na mwenyekiti wao kwa bunge la taifa ili kuidhinishwa.
Saba hao ni Erastus Edung Ethekon kama mwenyekiti wa tume hiyo ya IEBC, makamishna Anne Nderitu, Moses Mukwana, Mary Karen Sorobit, Hassan Noor, Francis Odhiambo, na Fahima Abdalla kuunda tume hiyo ya IEBC.