Business

Serikali Yalazimika Kufutilia Mbali Deni la Shilingi Bilioni 6 Kutoka Hazina ya Hustler

Published

on

Serikali sasa inasema italazimika kufuta deni la takriban shilingi bilioni 6 kutoka kwa Hazina ya Hustler, baada ya waliopewa mikopo kushindwa kulipa.

Katibu wa Idara ya Biashara Ndogo na za Kati, Bi Susan Mang’eni, amesema juhudi za kuwasaka waliokopa kisha kutotoroka na fedha hizo hazijazaa matunda, licha ya kuwa ni zaidi ya miaka miwili tangu kuanzishwa kwa hazina hiyo.

Kwa mujibu wa Mang’eni, ni Wakenya milioni 10 waliochukua mikopo lakini hawajarejesha, huku milioni 9 kati ya watu milioni 25 waliopokea fedha hizo wakilipa mikopo yao kama inavyotakiwa.

Ameeleza kuwa hali hiyo imeathiri kwa kiasi kikubwa uendelevu wa hazina hiyo, ambayo ililenga kuwainua wananchi kiuchumi kupitia uwezeshaji wa biashara ndogondogo.

Kutokana na hali hiyo, serikali sasa inawasihi wabunge kupitisha ombi la kutengewa shilingi bilioni 5 zaidi katika bajeti ya mwaka huu, ili kuendeleza shughuli za hazina hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version