News

Karua, Aomba Mahakama Kumuachilia Bessigye kwa Dhamana

Published

on

Kiongozi wa Chama cha People’s Liberation Party, PLP nchini Kenya Martha Karua, aliwasili nchini Uganda katika juhudi za kumuakilisha Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Bessigye anayetuhumiwa kwa kosa la Uhaini.

Bessigye alikamatwa nchini Kenya miezi sita iliyopita na kuwasilishwa Mahakamani licha ya hali yake ya kiafya kuonekana kudhoofika.

Akiwasilisha hoja yake Mahakamani, Karua ameitaka Mahakama hiyo kumuwachilia Bessigye kwa dhamana ikizingatiwa kwamba amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya siku 180 korokoroni bila ya kupata haki.

Kinyume na matukio ya hivi majuzi nchini Tanzania ambako alizuiliwa kwa muda wa saa sita na kisha kurejeshwa nchini Kenya, Kiongozi huyo chama cha PLP, alilakiwa Mahakamani kwa shangwe na nyimbo za ukombozi, kabla ya kupewa nafasi na Mahakama kuwasilisha hoja yake.

Safari yake ya kwenda nchini Uganda kuhudhuria kesi hiyo, inatokea wiki mbili tu baada ya kutibuka kwa jaribio lake la kutaka kumuakilisha kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, ambapo yeye na Wanaharakati wengine wa haki za binadamu walizuiliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kabla ya kurejeshwa nchini Kenya.

Tukio hilo limezua mashambulio makali ya mitandaoni miongoni mwa kizazi cha sasa cha Gen Z kuishtumu Tanzania kwa madai ya kudhuliwa kwa Mwanaharakati Bonifance Mwangi na mwenzake Agathar Atuhaire kutoka nchini Uganda.

Taarifa ya Eric Ponda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version