Sports
Alexander Trent Arnold Sasa Ni Mali Ya Madrid
Kilabu ya Real Madrid imtangaza kupata sahihi ya beki wa taifa la Uingereza na kilabu ya Liverpool Alexander Trent Arnold.
Miamba hao wa Uhispania inaaminika imelipa kima cha Euro milioni 10 kupata sahihi ya beki huyo ambaye amechezea Liverpool tangu utotoni akitokea kwenye academia ya kilabu hiyo.
Trent mwenye umri wa miaka 26 ametia wino mkataba wa miaka sita kilabuni humo inayomueka hadi mwaka 2031.
Makubaliano hayo yakiwa pia kwamba kilabu ya Madrid italipa mshahara wake wa miezi za June na Julai.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuvalia jezi la Los Blancos kwa mara ya kwanza katika fainali ya kombe la Dunia baina ya vilabu mwezi ujao Juni 14.