News

Owen Baya awataka wazazi walio na watoto wenye uatilifu kutowaficha

Published

on

Mbunge wa Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi Owen Baya ametoa wito kwa wenyeji wa kaunti ya Kilifi ambao wana watoto walio na uatilifu kujitokeza kuchukua basari za watoto wao ili wasome bila changamoto zozote.

Akizungumza mjini Kilifi wakati wa ugavi wa fedha za basari, Baya amesema serikali kuu huwa inatenga fedha maalumu za watu walio na uatilifu ingawa fedha huelekezwa katika matumizi mbadala ikizingatiwa kuwa walengwa huwa hawajitokezi kuchukua fedha hizo.

Baya pia amesema ikiwa wazazi watazingatia hilo itakuwa vyema kwani watoto hao watasoma na kuafikia ndoto zao za maisha.

Wakati huohuo, Baya ameitaka jamii kutowaficha walio na uatilufu akisema kila mtoto hapa nchini ana haki ya kupata elimu kulingana na katiba ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version