News

Zaidi ya familia 5,000 zahofia kufurushwa Matuga,Kwale.

Published

on

Zaidi ya familia elfu 5 eneo la Matuga kaunti ya Kwale zinahofia kufurushwa katika ardhi zao yenye zaidi ya ekari elfu 6.

Ardhi hizo zilikamilisha mda wa malipo ya kodi kwa waekezaji  tangu 2011  na kutarajiwa  kurejeshewa  wakaazi, japo zinadaiwa kuchukuliwa na mabwenyenye katika njia tatanishi.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Mwafitina Juma Bakari   wakaazi hao walisema kwamba licha ya tume ya ardhi nchini NLC kuzuru katika ardhi hizo mapema mwaka 2025, hadi sasa hakuna chochote kinachofanyika.

“Block ten kwanza walikuwa wanasema nyumba ni tatu wale mabwenyenye katika historia ambayo iko pale, lakini walipokuja NLC wakazunguka wakaona nyumba zaidi ya 300 wakashanga, halafu block hiyo hiyo tulikuwa tumeandikiwa barua na NCL mwaka 2011 kwamba tupimiwe na tuko na barua, lakini twashangaa mpaka sasa twashangaa haijapimwa na bwenyenye amerejea na kuchukua shamba”, walisema wakaazi.

Wakaazi hao walimtaka Rais Ruto kuingilia kati mzozo huo ili kuhakikisha jamii hizo zinapata haki.

Vile vile walieleza mahangaiko yao na kuashiria kuchoshwa na dhulma za kihistoria za ardhi.

“Watu wapwani tunadhulumika, watu wa Kwale tunadhulumika, watu wa Waa Ng’ombeni tunadhulumika, tunaomba aingilie kati kwa sababu hata hiyo mambo ya blue economy hatuna nafasi nayo kwa sababu mashamba bwenyenye anapima mpaka baharini, sasa hatua sehemu za kuegesha maboti, hatuna lolote”,waliongeza wakaazi.

Waliishikilia kuwa iwapo suala hilo halitaangaziwa huenda wakalazimika kuandamana hadi ofisi kuu za tume ya ardhi NLC jijini Nairobi kudai haki zao.

Taarifa ya Mwanahabari wetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version