News
Karisa Nzai:Gachagua anaendeleza siasa za ukabila
Mshauri wa rais katika maswala ya kisiasa Karisa Nzai amemkosoa kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua kwa madaia ya kuendeleza siasa za ukabila.
Akizumgumza katika hafla iliyoileta pamoja jamii ya Kipsigis kaunti ya Mombasa, Nzai alimtaja Gachagua kama kiongozi ambaye nia yake kuu ni kuwagawanya wakenya kwa msingi ukabila na wala sio mshikamano wa kitaifa.
Nzai alisema siasa anazoendeleza Gachagua zimepitwa na wakati, na kuwasihii wakenya kumuunga mkono rais William Ruto ili atimize ajenda zake kwa wakenya.
Kwa upande mwenyekiti wa jamii ya Kipsigis tawi la Mombasa Earnest Kiptoo alizitaka jamii zote kuzingatia mshikamano wa kitaifa ili kuendeleza maendeleo ya nchi, na kupuuza siasa za mgawanyiko zinazoendelezwa na upinzani
Taarifa ya Joseph Jira.