News

Karisa Ngirani: Baadhi ya wadi Ganze zimetelekezwa na Kaunti

Published

on

Mwakilishi wadi ya Ganze Karisa Ngirani anadai baadhi ya wadi ndani ya eneo bunge la Ganze zimekuwa zikitelekezwa katika maswala ya ugavi wa raslimali katika kaunti ya Kilifi.

Katika mahojiano na COCO FM, Ngirani alisema wamekuwa wakishinikiza serikali kuangazia matatizo ya wakaazi maeneo hayo ili kuhakikisha wakaazi wanafaidi miradi ya maendeleo.

Ngirani aliadai aliwasilisha hoja katika bunge la kaunti kuangazia usawa wa ugavi wa raslimali, baada ya baadhi ya wawakilishi wadi kulalamikia suala hilo.

Kulingana na mwakilishi huyo wa wadi hoja hiyo ilitupiliwa mbali licha ya kukubaliwa na wananchi baada ya kuandaa vikao vya kukusanya maoni ya umma.

“Nilikuja na hoja ambayo inaitwa “equitable bill” inaangazia usawa wa raslimali vile tunazigawanya kwa kila wadi, manake nilipoingia pale wawakilishi wengi walikuwa wanalalamika, ukiangalia ni kweli, unaangalia labda kuna mwakilishi wadi ambaye yuko karibu na gavana, huyo unapata bajeti ikitengenezwa ako na asilimia kubwa sana, lakini naskia imerejeshwa na viongozi wa juu”,alidai Ngirani

Vile vile Ngirani alidokeza kuwa suala la uhaba wa maji safi ya matumizi kwa wakaazi wa Ganze limesalia changamoto licha ya pesa zilizotengewa miradi ya maji kutolewa kwenye bajeti ya ziada.

Akiangazia masuala ya mazingira Ngirani alisema wanashirikiana na mashiriki mbali mbali kufanikisha utunzaji mazingira katika kaunti ya Kilifi, na wanapanga  kuwasilisha hoja bungeni itakayotoa fursa kwa wananchi ndani ya kaunti, kutenga sehemu ya ardhi ili kuwezesha upanzi wa miti.

Alidokeza kuwa idara ya mazingira imekuwa ikitengewa mgao wa chini mno wa fedha hali ambayo imekuwa vigumu kutekeleza miradi ya kuboresha mazingira ili kukabili mabadiliko ya tabia nchi.

“Saa hii tunasukuma tuweke mswada kwamba angalau kila eneo liwe na msitu, litenge sehemu kadhaa ya ardhi ili iwe inapandwa miti iwe ni kama shamba ambalo wananchi wanawezapeana”, alisema Mwakilishi huyo wa wadi.

Taarifa ya Mwanahabari wetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version