News

Seneta Miraj apiga jeki mpango wa vitambulisho maalum Mombasa

Published

on

Seneta mteule katika kaunti ya Mombasa Miraj Abdillahi ameunga mkono mpango wa gavana wa kaunti hiyo Abdulswamad Shariff Nassir wa kuzindua vitambulisho maalumu kwa wenyeji wa kaunti ya Mombasa, ili wenyeji waweze kupata huduma mbalimbali kwa gharama nafuu na kwa urahisi.

Abdillahi ambaye alikuwa akizungumza katika eneo la Shika Adadu eneo  bunge la Likoni, kwenye hafla ya ugavi wa chakula, alisema hilo litawapunguzia wenyeji mahangaiko ambayo wamekuwa wakiyapitia kutokana na gharama za juu za matibabu katika kaunti ya Mombasa.

Kulingana na Miraj Abdillahi, wenyeji wamekuwa wakihangaika kutokana na gharama ya juu ya matibabu, chanzo kikuu kikiwa ni wawakilishi wa wadi wa kaunti ya Mombasa.

“Tumekuwa tukilia ya kwamba bili za hospitali ziko juu, si fitina na si siasa ikiwa mnataka bei ya huduma ya Coast General kushuka chini ongeeni na wawakilishi wa wadi wenu’’, Alisema Abdillahi.

Wakati huo huo, Abdillahi alitoa wito kwa wawakilishi wa wadi kutathmini sheria ambazo walibuni ili kupatikane mwafaka.

Haya yanajiri huku mvutano ukiendelea kushuhudiwa kati ya bunge la kaunti hiyo na serikali ya kaunti ya Mombasa kuhusiana na suala hilo.

Taarifa ya Janet Mumbi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version