Business

Waziri Miano Asisitiza Ushirikiano Kati ya Serikali na Sekta Binafsi Katika Kuimarisha Utalii

Published

on

Waziri wa Utalii, Bi Rebecca Miano, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi katika kuandaa mpango wa pamoja wa kusaidia biashara na maeneo ya utalii nchini.

Akizungumza na wanahabari, Waziri Miano alisema kuwa sekta ya utalii nchini bado inakumbwa na changamoto mbalimbali, hivyo kuna haja ya kuweka mikakati madhubuti ili kuiimarisha na kuiwezesha kuchangia zaidi kwenye uchumi wa taifa.

Aidha, Waziri huyo alieleza kuwa kuna umuhimu wa kuwa na mfumo bora wa kudhibiti na kuboresha ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta ya utalii. Alisema mfumo huo unapaswa kuzingatia pia mabadiliko ya tabianchi, ambayo kwa sasa yanaathiri pakubwa shughuli za utalii duniani.

Bi Miano alihitimisha kwa kusema kuwa kwa kuwepo kwa ushirikiano thabiti kati ya pande zote, sekta ya utalii inaweza kuwa chombo kikuu cha kukuza uchumi na kutoa ajira kwa maelfu ya Wakenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version