Business
Wakulima wa Mahindi Chonyi Wakadiria Hasara Kutokana na Mvua Kubwa
Baadhi ya wakulima wa mahindi katika eneo la chonyi kaunti ya kilifi wanakadiria hasara kutokana na mvua nyingi ambayo inaendelea kunyesha maeneo mengi nchini.
Kulingana na wakulima hao hasa ambao mashamba yao yako karibu na mito mahindi waliyopanda hayastahimili mvua nyingi hivyo kuwasababishia hasara kutokana na kuharibika .
Wanasema mahindi mengine yamesombwa na maji hali ambayo imeawasabashia hasara na kuitaka serikali kuwasambazia mbegu ambazo zinaweza kustahimili mvua nyingi ili waweze kuendeleza kilimo biashara bila changamoto zozote ikizingatiwa wanategemea kilimo kujikimu kimaisha.
“ mashamba yamejaa maji kila mahali hali ambayo imefanya mahindi kuoza na hata kuchomeka hasa sisi ambao mashamba yetu yako karibu na mito hatutapata chocote kabisa”