Business
Kenya kuzindua utalii wa anga (Astro-tourisim)
Kenya itakuwa mwenyeji wa uzinduzi wa utalii wa anga(Astro-tourisim) katika kaunti ya Samburi Septemba 7, 2025, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha na kubadilisha aina za utalii nchini.
Uzinduzi huo unaendana sambamba na tukio la mwezi kupatwa maarufu kama Blood moon ambapo litaanza saa mbili na nusu usiku wa septemba 7, 2025, na kudumu kwa dakika 82.
Mpango huu wa kipekee unalenga kuifanya Kenya kuwa kivutio kikuu cha wapenzi wa sayansi ya anga na wasafiri wa kimataifa wanaopenda maajabu ya siri.
Kwa mujibu wa shirika la Magical Kenya, tajriba hii ya anga inalenga kutumia mazingira ya kipekee ya nchi kufungua ukurasa mpya na endelevu wa utalii.
Waziri wa utalii na wanyama pori Rebecca Miano atakuwa mgeni rasmi akiandamana na wageni wa kimataifa katika hafla hiyo itakayofanyika katika Sopa Lodge kwenye hifadhi ya kitaifa ya Samburu.
Taarifa ya Joseph Jira