News
Visa vya mauji ya wazee vyapungua Kilifi
Idara ya usalama kaunti ya Kilifi imeripoti kupungua kwa visa vya mauaji ya wazee, hatua inayotajwa kuwa mafanikio makubwa katika juhudi za kukomesha uhalifu huo unaochochewa na imani potovu za uchawi.
Kwa mujibu wa kamishna wa kaunti hiyo, Josephat Biwot, idadi ya wazee waliouawa mwaka jana ilishuka hadi watu 12, ikilinganishwa na mwaka wa 2023 ambapo visa 60 vya mauaji viliripotiwa.
Biwot, alisema mauaji hayo hayahusiani moja kwa moja na uchawi kama inavyodhaniwa, bali yanatokana na migogoro ya ardhi, huku ndugu na jamaa wa karibu wa waathiriwa wakitajwa kuwa wahusika wakuu.
“Nikija Kilifi 2023 tulikuwa tunapoteza wazee karibu 60 kwa mwaka, lakini mwaka jana kwa bahati mbayu tu tulipoteza wazee 12 pekee, na wale walikufa kulishika washukiwa wote”,alisema Biwot.
Kamishna huyo aliwaonya vijana wanaojihusisha na vitendo hivyo, akisema serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yao.
“Tunaomba vijana wetu hii ni laana, sasa wewe unaua babayako kwa sababu ya shamba, wewe utaishi namna gani? Kwa sababu waweza kuua baba uuze shamba, ununue pikipiki ndio unaona ajali nyingi”, aliongeza Biwot.
Taarifa ya Mwanahabari wetu.