News
Viongozi pwani waombwa kuwajibikia pesa za wavuvi
Kamati ya Bunge la kitaifa kuhusu uchumi wa bahari imewataka viongozi wa pwani kuhakikisha fedha zinzotolewa na serikali kuu pamoja na mashirika mengine kwa ajili ya miradi ya uvuvi zinatumika ipasavyo kuwanufaisha wavuvi moja kwa moja.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, mbunge wa Marakwet Mashariki David Bowen, alisema licha ya mabilioni ya pesa kuelekezwa katika sekta hiyo, jamii nyingi za wavuvi bado hazijafaidika kama inavyotarajiwa.
Kwa upande wake mbunge wa Malindi Amina Munyazi, alisema kama viongozi hawana taarifa kamili kuhusu fedha hizo, na akasisitiza haja ya ushirikiano wa karibu kati ya serikali, viongozi na mashirika ya maendeleo.
Baadhi ya wavuvi walilalamikia kutotimizwa kwa ahadi, huku miradi mingi ikisalia kwenye makaratasi bila utekelezwaji mashinani.
Taarifa ya Mwanahabari wetu.