Business
Wafanyabiashara Wataka Soko la Matano Mane Kufunguliwa Rasmi
Wito unazidi kutolewa kwa serikali ya kaunti ya kilifi kuhakikisha kuwa soko lililojengwa miaka 15 eneo la Matano mane linafunguliwa ili kuwawezesha kuendeleza biashara zao bila changamoto.
Kulingana na Ngari Kombe ambaye ni moja wa wafanyibiashara eneo hilo shughuli za kibiashara katika eneo hilo ziko chini kwani punde mvua inaponyesha wafanyibiashara wanasusia kwenda sokoni wakihofia bidhaa zao kuharibika.
Akizungumza na meza yetu ya biashara Kombe amesema kuwa kwa sasa wafanyibiashara wanahangaika ili hali kuna soko ambalo wanaweza kuendeleza biashara zao bila changamoto.
Sasa Kombe amewataka viongozi wa eneo hilo kufungua soko hilo rasmi ili kuwawezesha wafanyibiashara kuendeleza shuhuli zao ikizingatiwa kuwa wengi wanategemea biashara kujinua kiuchumi.
“Soko lilijengwa kitambo liko hapo milango imefungwa wafanyibiashara wanahangaika ili hali kuna mahali wanaweza fanyibiashara hapo.
“Tunaomba serikali ya kaunti ifungue hili soko ili wafanyibiashara tusaidike”