Sports
Kiungo Wa Junior Stars Aldrine Kibet Ni Mali Ya Celta Vigo
Nyota wa timu ya Taifa ya soka Harambee Stars vijana Chipukizi ‘Junior Stars’ Aldrine Kibet sasa amejiunga rasmi na kilabu ya Celta Vigo nchini Uhispania.
Hii ni baada ya kutia Saini mkataba na klabu hiyo inayomueka Uhispania kwa misimu minne.
Kiungo huyo wa Junior Stars, ametangazwa rasmi kujiunga na Klabu hiyo ya Celta Vigo kwa mkataba wa miaka minne hadi mwaka 2029.
Kibet mwenye umri wa miaka 19 anajiunga na klabu hiyo baada ya kupitia mafunzo ya mchezo wa kandanda katika Akademia ya Nasty Sports nchini Uhispania alichojiunga nacho miaka miwili iliopita, punde tu alipomaliza masomo yake katika shule ya Upili Ya St. Anthony Kitale nchini Kenya.
Mchezaji huyo pia amechezea Junior Stars katika mashindano ya CECAFA humu nchini na Tanzania mwaka jana na mwaka 2023 na pia kombe la bara Afrika kwa Chipukizi mwezi Mei mjini Cairo Misri.