Entertainment
Verse Smart, Rojo Mo Amsifia Nyota Ndogo
Wimbo mpya wa “BARAKA” unaowakutanisha Rojo Mo, Nyota Ndogo, Chikuzee, na Cannibal The Chosen One unaendelea kumwagiwa sifa kwenye mitandao ya kijamii kwa kukutanisha lejendari wa mziki wa Pwani – si tu kwa beat kali na ujumbe wake wa kusifu Mungu.
Tukio la hivi punde ni Rojo Mo kusifia verse ya Nyota Ndogo kwenye wimbo huo. Rojo Mo, mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa katika scene ya muziki, alitoa maneno haya kupitia ukurasa wake wa Facebook:
“Leo ni NYOTA NDOGO Big up kwa verse smart 🌸 Maua yako pokea #BARAKA”
Rojo Mo amekuwa akiachia picha za walioshirikiana kwenye wimbo akiskuma link ya wimbo wao; alianza na Chikuzee na sasa amefika kwa Nyota Ndogo. bila shaka kesho tutaona picha ya Canibal aliyemtakia heri kwenye siku ya kuzaliwa Juni tarehe tatu.
Katika wimbo huu, Nyota Ndogo anaingia akisifia penzi analolipata kutoka kwa Mungu kabla ya Chikuzee kuchukua hatamu. Ushirikiano wa wasanii hawa wanne – Rojo Mo nyota wa hits, Nyota Ndogo mkwasi wa sauti kutoka Mombasa, Chikuzee mwenye uandishi wa kina na sauti ya kipekee, pamoja na Cannibal The Chosen One, mkali wa mtindo huru (freestyle) – umeleta ladha ya kipekee kwenye track hii.
Kando na ubunifu wa kisanaa, wimbo wa BARAKA unajitokeza pia kama aina ya wimbo wa kusifu na kutoa shukrani – sio kwa mtazamo wa kidini pekee, bali wa maisha ya kila siku. Wasanii wote wanne wanaelezea jinsi Mungu anavyowafungulia milango ya baraka na ufanisi. Wanarejesha sifa kwa Mungu kwa matendo yake makuu. Maneno yao yanagusa roho na kutufundisha kuwa kila hatua ya maendeleo si tu baraka inayostahili kusherehekewa bali pia ni fursa ya kumpa Mungu shukurani.
Huu ni wimbo unaotufundisha kuona uzuri hata katika magumu, na kukumbuka kusema “asante” – kwa uhai, kwa familia, kwa kipaji, na hata kwa yale tuliyoyapitia. Kwa namna ya kipekee, BARAKA inakuwa sauti ya sifa, sala ya mitaani, na salaam ya matumaini kwa yeyote anayeisikiliza akiwa kwenye safari yake ya maisha.
Mashabiki mitandaoni wameonyesha mapenzi yao kwa wimbo huu, wakisifia utunzi, video ya kuvutia, na “chemistry” ya wasanii waliokutana. Lakini zaidi.
Katika dunia ya muziki, si kila wimbo ni wa kawaida. Wimbo wa “BARAKA” ni reminder kwamba muziki unaweza kuwa tiba, kuwa nuru, na kuwa silaha.