News

Polisi:Mauaji ya wazee Kaloleni-Kilifi yamedhibitiwa

Published

on

Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Kaloleni kaunti ya Kilifi, Kyalo Kaloki amewapongeza wenyeji kwa juhudi ambazo wamekuwa wakiweka kudhibiti mauaji ya wazee kwa tuhuma za uchawi.

Kaloki ambaye alikuwa akizungumza katika eneo la Gotani, wadi ya Kayafungo, aliitaka jamii eneo hilo pia kushirikiana na afisi za machifu ili kupata mwafaka wa migogoro ya mashamba ambayo imekithiri maeneo hayo.

Kaloki pia alisema maafisa wa polisi wamekuwa wakipokea kesi za mashamba kwa wingi.

Vilevile, Kaloki alisema ni kupitia ushirikiano ndipo mizozo ya ardhi itadhibitiwa vilivyo.

“Sasa ile kesi naomba tupunguze pia ni kesi ya mashamba,mkikosana na jirani yako hapana kukimbia kwa kituo cha polisi, eti unaenda kumshtaki amekutishia maisha, Ita wazee wenzenu, kaeni chini mtatue’’, alisema Kaloki.

Eneo la pwani limekuwa kishuhudia visa vya wazee kuawa kwa tuhuma za ushirikina, huku baadhi yao wakilazimika kukimbilia usalama wao katika makao ya kuhifadhi wazee.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version