News

Bunge la kaunti ya Kilifi kuchagua spika mpya

Published

on

Bunge la kaunti ya Kilifi linatarajiwa kumchagua spika mpya Julai 21,2025.

Hii ni baada ya Teddy Mwambire kubanduliwa uongozi na wawakilishi wadi Juni 30 2025 kupitia kura ya maoni.

Mwambire alibanduliwa mamlakani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na ukiukaji wa katiba.

Shughuli hiyo inafanyika licha ya mahakama nchini kumwagiza Mwambire kuendelea kushikilia wadha huo.

Miongoni mwa wanaowania wadhifa huo ni pamoja na wakili Faith Zawadi Kingi, Tendai Mtana Lewa, Catherine Kenga, na Mazera Shadrack.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version