News

Paul Katana:Viongozi wacheni siasa za chuki

Published

on

Mbunge wa Kaloleni kaunti ya Kilifi Paul Katana ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kujiepusha na siasa ambazo huenda zikasababisha chuki miongoni mwa wenyeji.

Akizungumza katika eneo la Gotani, Katana alisema ili kuimarisha taifa la Kenya kimaendeleo, ni lazima kuwe na umoja na amani ili kuafikia hilo.

Katana alisema ni jukumu la viongozi kuwa katika mstari wa mbele kudumisha amani na sio kuwachochea wananchi ili kuzua vurugu nchini.

“Nchi hii itajengwa wakati kuna amani, hata tukiwa na tofauti zetu za kisiasa, tukiongea na wananchi tuwaambie sera zetu, tusiwachochee kisiasa’’,alisema Katana.

Wakati huohuo, Katana aliwataka viongozi kukoma kuingiza siasa kwenye hazina ya ustawishaji maeneo bunge-CDF na kuwashinikiza kushirikiana ili kuhakikisha fedha hizo zinawafaidi wakenya.

“Pesa ya CDF ndio pesa pekee yake inayomgusa mwananchi moja kwa moja, lakini kuna watu ambao wanasema CDF itolewe katika nchini yetu’’, aliongeza Katana.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version