News

Mwanaharakati Boniface Mwangi kushtakiwa kwa ugaidi

Published

on

Mwanaharakati Boniface Mwangi anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu 21 Julai, 2025 kujibu mashtaka ya kufanikisha ugaidi.

Maafisa wa upelelezi wa jinai walisema kuwa Mwangi alipatikana na risasi na vitoa machozi wakisema kuwa ni ushahidi kuwa alihusika na ugaidi wakati wa maandamano ya Juni 25, 2025.

Wanaharakati walilaani kukmatwa kwa Mwangi wakisema madai ya polisi hayana msingi wowote.

Walishinikiza polisi kumwachilia Mwangi na kupinga tuhuma dhidi yake, huku wakisema ni mbinu za serikali kukandamiza sauti zinazoikosao.

Mwashirika 61 ya kutetea haki za binadam yalikosa hatua ya Mwangi kukamatwa, yakionya kuhusu mtindo unaoendelea wa kuwakamata kiholela na kuwafungulia mashtaka ya uongo wakosoaji wa serikali.

Yanasema hali hiyo ni tisho kwa demokrasia ya Kenya.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version