News

Polisi wamewakamata washukiwa 6 wa uhalifu, Mombasa

Published

on

Maafisa wa Idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI kaunti ya Mombasa wamewakamata washukiwa 6 wa uhalifu wa mtandao wanaoshukiwa kuhusika na ulaghai kwa kutumia teknolojia ya kubadilisha namba za simu (caller ID spoofing), kwa lengo la kuwahadaa wananchi na kuwaibia pesa.

Washukiwa hao ni pamoja na Fortune Muthina Kinyanzui almaarufu Albanas Kyalo, Ruel Kipkoech Yator almaarufu Papa Ruel, Laban Kipkirui Koech, Weldon Kipyegon Rono, Towet Kipkorir Alphonce na Kelvin Kipyegon Koech.

Washukiwa hao wanadaiwa kuwapigia simu waathiriwa wakijifanya kuwa wahudumu wa wateja wa benki au kampuni za simu na kisha kuwahadaa watoe taarifa zao kama namba za vitambulisho, nambari za siri (PIN) na taarifa nyingine muhimu za kifedha ambazo walizitumia kuiba pesa kutoka kwa akaunti zao.

Inadaiwa kuwa Fortune Muthina, ambaye ni kiongozi wa genge hilo ndiye anayemiliki mfumo huo wa kudanganya namba za simu, ambayo alikuwa anakodishia matapeli wengine kuitumia kwa ada ya zaidi ya shilingi laki tano.

Washukiwa hao walikamatwa katika nyumba waliokuwa wamekodi na kujificha ili kutekeleza uhalifu huo ambapo maafisa wa polisi walifanikiwa kupata simu 19, laini za simu kutoka mitandao tofauti ya mawasiliano pamoja na daftari lenye majina na taarifa za watu wanaoshukiwa kuwa waathiriwa.

Taarifa ya Mwanahabari wetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version