Sports
Kenya Pipeline Yaanza Kwa Kishindo Fainali Ya Voliboli
Kilabu ya Kenya Pipeline ilianza kwa kishindo fainali ya taji la akina dada mchezo wa voliboli mashidano yanayondelea uwanjani Kasarani Indoor Arena jijini Nairobi.
Hii ni baada ya vipusa hao chini ya kocha Godfrey Omondi kuwatandika wenzao DCI seti 3-0 mechi ya ufunguzi uwanja huo ukifurika hadi pomoni.
Kikosi hicho kilishinda mechi hiyo kwa seti 25-19,25-20,25-14 na kuibuka na ushindi huo mnono kabila ya mechi ya pili jumamosi.
Nahodha wa KPC Gladys Ereng amesema kwamba mechi haikua rahisi kwani DCI walikua vizuri ila walipambana kwa ushindi huo.
“DCI ni timu nzuri walicheza vizuri kipindi cha kwanza kwani tulianza kwa utepetevu ila tukazungumza na kujikusanya vyema na kupata ushindi huo muhimu kwetu.”
Kwa Upende wake kocha wa DCI Patrick Sang amedokeza kwamba hakucheza kwa umakinifu waliotarajia;”Hatukucheza kwa mipangilio yetu mazungumzo pamoja na utulivu haikuwepo lakini ndio hali ya mchezo nipongeze wenzetu.”
Kilabu ya General Service Unit (GSU) upande wa wanaume ilianza vema kusaka taji la upande wa Wanaume baada ya kushinda mechi ya mkondo kwanza sati 3-0 katika uwanja huo huo.
Hii ni baada ya kuwatandika Kenya Ports Authority (KPA) seti 3-0 za 25-15,25-22,30-28