News

Gachagua, amkosoa Rais Ruto kwa madai ya uongozi duni

Published

on

Viongozi wa upinzani nchini wakiongozwa na Kinara wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua waliendeleza kampeni za Wantam dhidi ya rais William Ruto wakielenga uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027.

Wakazingumza wakati wa ziara yao ya kisiasa katika eneo la Pwani, Kalonzo alimkosoa rais Ruto akisema ameshindwa kuongoza taifa hali na kuendelea kuwanyanyasa vijana wa Gen Z kwa kuwateka nyara kiholela.

Kalonzo hata hivyo alidai kwamba serikali ya Kenya kwanza ina malengo fiche dhidi ya Bandari ya Mombasa, akisema kama wapinzani watahakikisha serikali ya rais Ruto ina hudumu kwa muhula moja pekee.

“Rais Ruto alishindwa kuongoza nchi na kuendelea kuwanyanyasa wakenya hasa vijana wa Gen Z kwani tumeshuhudia utekaji nyara wa kiholela na hata bandari ya Mombasa wako na malengo fiche na hiyo”, alisema Kalonzo.

Kwa upande wake aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na ambaye pia ni Kinara wa Chama cha DCP, amemkosoa rais Ruto na Katibu wa Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli kwa kuwahadawa wakenya na kusambaratisha uchumi wa nchi pamoja na kufuja fedha za hazina ya NSSF huku Atwoli akilinyamazia suala hilo.

“Pesa ya NSSF imechukuliwa na Rais Ruto na kuendelea kujenga barabara na Bomas hiyo ni kinyume na sheria na hatutakubali na yule kiongozi wa kutetea wafanyikazi Atwoli amenyamaza ama wamekula hiyo pesa pamoja”, alisema Gachagua.

Upinzani waendeleza kampeni za Wantam

Hata hivyo viongozi walioandamana na Kalonzo katika ziara hiyo ya kisiasa eneo la Pwani wakiongozwa na Mgombea wa kiti cha ubunge wa eneo bunge la Magarini Furaha Chengo Ngumbao, walisema serikali imesheheni wizi wa mashamba ya wakaazi wa Pwani na kudia kwamba mamlaka yote yako nchini ya wananchi.

Wengine walioandamana na Kalonzo ni pamoja na Naibu Kinara wa DCP Cleophas Malala, Mbunge wa Wundanyi Danson Mwashako, Seneta wa Kisii Richard Onyonka miongoni mwa viongozi wengine.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version