News

Polisi Wamemkamata Mchungaji Tata, Chakama

Published

on

Maafisa wa usalama kaunti ya Kilifi wanamzuilia mchungaji tata Abel Kahindi Gandi wa kanisa la New Foundation lililoko Chakama eneo bunge la Magarini kuhusiana na vifo tatanishi vya wafuasi wake.

Kulingana na maafisa polisi, wanamchunguza mchungaji huyo kubainisha usajili wa kanisa lake pamoja na waliopoteza wapendwa wao kuandikisha taarifa kwa polisi.

Naibu Kamishna wa eneo la Kilifi Kaskazini Samuel Mutisya amesema wanatilia shaka masomo yake ya Kitheolojia ambayo yangemuwezesha kuendelea na huduma za mahubiri yake.

Wakati huo huo Mutisya amesema iwapo mchungaji huyo atapatikana bila hatia atawekwa huru na iwapo itabainika kwamba amekuwa akiendesha huduma zake kinyume na sheria basi atakabiliwa na mkono wa serikali.

Mchungaji Gandi pia anadaiwa kuwalazimisha wafuasi wake kupanda juu ya mti uliyoo nje ya kanisa lake, akidai ni mti wa uzima na ungetatua matatizo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version