News
Idara ya usalama pwani yakemea siasa za chuki
Idara ya usalama eneo la Pwani imeonya viongozi na wanasiasa dhidi ya kuzua semi za uchochezi ambazo huenda zikachangia vurugu eneo hilo.
Kamishna wa jimbo la Pwani Rhoda Onyancha alitahadharisha viongozi hasa katika kaunti ya Tanariver dhidi ya kuvuruga amani akisema eneo hilo kwa sasa liko salama baada ya kushuhudia machafuko ya kikabila mwaka jana.
Onyancha alisistiza wakaazi kuendelea kudumisha amani na mshikamano ili kuboresha mazingira ya maendeleo eneo la Pwani.
“Tunajua kulikuwa na mambo hapa na pale mwaka wa 2023/24, lakini mwaka huu tumekuwa watulivu sana, na ningependa kuwasihi kwamba tuendelee kuweka huo utulivu vile vingozi wanasema”, alisema Onyancha.
Vile vile aliwasihi viongozi kushirikiana na serikali kujenga ofisi za maafisa wa utawala mashinani wakati serikali ikiendelea kubuni sehemu za utawala.
Taarifa ya Joseph Jira