News

Watu wawili wafariki kutokana na Mpox Mombasa

Published

on

Serikali ya kaunti ya Mombasa imethibitisha vifo vya watu wawili kutokana na ugonjwa wa Mpox, huku maambukizi mapya yakiendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo.

Msimamizi mkuu wa Idara ya afya kaunti ya Mombasa, Dkt Mohammed Hanif, alisema tangu ugonjwa wa Mpox uripotiwe humu nchini Julai 31, 2024, jumla ya visa 226 vimeripotiwa ikiwemo vifo 4, huku kaunti ya Mombasa ikiwa miongoni mwa kaunti 21 zilizoathirika.

Dkt Hanif alisema kisa cha kwanza cha Mpox kaunti ya Mombasa kiliripotiwa Septemba 3, 2024, na kufikia sasa watu 159 wamefanyiwa vipimo, ambapo 98 kati yao wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza na Wanahabari, Dkti Hanif alisema kati ya wagonjwa hao, 24 wamelazwa katika kituo cha kutenga na kutibu wagonjwa katika kituo cha afya cha Coast General eneo la Utange huku akisema kumekuwa na ongezeko la maambukizi mapya mwezi ya Juni na Julai.

“Hii ugonjwa iko na tayari watu 159 wamefanyiwa vipimo ambapo 98 kati yao wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo na kati ya wagonjwa hao, 24 wamelazwa katika kituo cha kutenga na kutibu wagonjwa katika kituo cha afya cha Coast General eneo la Utange”, alisema Dkt Hanif.

Kwa upande wake, Afisa wa Shirika la Stawisha Pwani, Vinceny Omoth, aliwataka wakenya hususan wale wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Mpox.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version