Sports

Chelsea Yafunguliwa Mashtaka kwa Ukiukaji wa Kanuni 74 za Malipo kwa Mawakala

Published

on

Kilabu ya Chelsea imefunguliwa mashtaka na Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) kwa madai ya kukiuka kanuni 74 zinazohusiana na malipo kwa mawakala kati ya mwaka 2009 na 2022.

Mashtaka hayo yanalenga zaidi matukio yaliyotokea kati ya msimu wa 2010-11 hadi 2015-16.

Ukiukaji unaodaiwa unahusu mawakala, wapatanishi na uwekezaji wa watu wa tatu kwa wachezaji.

Chelsea wamepewa muda hadi tarehe 19 Septemba kujibu mashtaka hayo.

Kuna adhabu mbalimbali zinazoweza kutolewa dhidi ya Chelsea, ikiwemo faini, marufuku ya usajili na kupunguzwa pointi. Hata hivyo, kiwango cha juu cha ushirikiano wa klabu hiyo kitapewa kipaumbele katika kuamua uamuzi wa mwisho.

Mwenye biashara wa Kirusi Roman Abramovich alikuwa mmiliki wa klabu hiyo kuanzia mwaka 2003 hadi 2022. Aliiuza Chelsea kwa muungano ulioongozwa na mwekezaji Mmarekani Todd Boehly na kampuni ya uwekezaji binafsi Clearlake Capital.

Mnamo Julai 2023, Chelsea walitozwa faini ya pauni milioni 8.6 na Uefa kwa kukiuka kanuni za Financial Fair Play kutokana na “kuwasilisha taarifa zisizokamilika za kifedha” kati ya mwaka 2012 na 2019.

Ukiukaji huo ulibainishwa na uongozi mpya wa Stamford Bridge kufuatia mauzo ya klabu hiyo mnamo Mei 2022.

Kama ilivyoripotiwa na BBC Sport mnamo Oktoba 2023, usajili uliomhusisha Samuel Eto’o na Willian ulikuwa sehemu ya uchunguzi wa Ligi Kuu ya Uingereza kuhusu ukiukaji wa kanuni za kifedha na Chelsea.

Wachezaji hao wote wawili walijiunga na klabu hiyo wakati Abramovich akiwa bado anamiliki, wakitokea klabu ya Urusi Anzhi Makhachkala mnamo mwaka 2013.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version