International News

Kampeni za uchaguzi mkuu za shika kasi Tanzania

Published

on

Mgombea wa wadhfa wa Rais wa Jamhurui ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa chama cha Mapinzudi CCM taifa Dkt Samia Suluhu Hasssan anaendeleza kampeni za uchaguzi mkuu kwa chama hicho.

Rais Samia Suluhu, na mgombea mwenza Emmanuel Nchimbi kutoka chama tawala CCM, wamo katika harakati za kuwashawishi wapiga kura ili kuwachagua kuliongoza taifa hilo kwa awamu nyingine ya miaka mitano ijayo.

Siku ya Alhamis tarehe 11 Septemba 2025, Rais Samia Suluhu alifanya mkutano mkubwa wa siasa katika eneo la Urambo mkoani Tabora, ambako alizungumzia zaidi ufanisi wa maendeleo akisema umetokana na utawala bora wa chama cha Mapinduzi (CCM).

Miongoni mwa hayo ni kuboreshwa kwa muundo misingi ya barabara, afya na ustawi wa uchumi na biashara, na kutaja kimakusudi zao la Tumbaku linalokuzwa kwa wingi mkoani Tabora.

Rais Samia alisema kuwa kunaongezeko kubwa la pato linalotokana na zao la Tumbaku ambapo sasa linauzwa kwa dola 2.5 kutoka bei ya zamani ya dola 1 kwa tani moja.

Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Tanzania katika mji wa Urambo mkoa wa Tabora {picha kwa hisani}

Kwa upande wake, Mgombea mwenza Emmanuel Nchimbi alikuwa katika mkoa wa Katavi, kusasambua yale serikali ya Mama Samia Suluhu imepanga kuyatimiza punde tu itakapochaguliwa kuwaongoza Watanzania.

Tanzania inaingia kwenye kampeni za uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba, 29 2025.

Mpinzani wake mkuu Tundu Lissu anaendelea kuzuiwa jela, kwa tuhma za uchochezi na uhaini.

Taarifa ya Eric Ponda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version