Sports

Wanandondi Mombasa Kuingia Kambini

Published

on

Chama cha Ndondi kaunti ya Mombasa (MCBA) kinatarajia kuanza rasmi kambi ya mafunzo, hii leo  katika taasisi ya Alliance Française huko Nyali, kama sehemu ya maandalizi kuelekea ligi ya kitaifa ya ndondi inayotarajiwa kuanza tarehe 17 hadi 19 Julai mwaka huu.

Kambi hiyo  italeta pamoja wakufunzi 10 kutoka jijini Mombasa wakishirikiana na wataalam wawili wa kimataifa ambao ni Franck Petitjean bingwa wa zamani wa Ulaya na bingwa wa mara nne wa Ufaransa pamoja na Valentino Gargiulo mtaalamu wa hali ya mwili kwa wanamichezo

Kambi hii inazinduliwa juu ya mafanikio ya mradi wa ndondi mashinani, mradi wa pamoja kati ya Kenya na Ufaransa uliozinduliwa mwezi Mei mwaka huu, ukiwa na lengo la kuwapa vijana mafunzo, kuwawezesha makocha, na kuandaa mabondia mahiri kwa ushindani wa kimataifa.

Kwa sasa, Mombasa inaweka mikakati ya kuibuka na ushindi katika Ligi ya Kitaifa, kambi hii ikiwa ni sehemu ya safari hiyo ya mafanikio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version