News

Maabara ya siri ya dawa za kulevya yafichuliwa Kwale

Published

on

Idara ya usalama katika kaunti ya Kwale imefichua maabara ya siri ya dawa za kulevya katika kijiji cha Mwabungo eneo la Ukunda.

Kulingana na vyanzo vya usalama maabara hiyo iko ndani ya shamba la ekari moja lililoweza kuunganishwa na ukuta wa lango lenye ulinzi mkali.

Baada ya siku kadhaa za upelelezi wa kisiri na ukusanyaji wa taarifa za kiinteligensia, kikosi cha kitengo maalum cha kupambana na ulanguzi wa dawa za kulevya kwa ushirikiano na maafisa wa polisi kiliendesha msako wa kushtukiza eneo hilo.

Maafisa waliwakamata watu wawili mmoja akiwa raia wa Italia mwenye umri wa miaka 37, mwengine akiwa ni Moses Nanoka.

Vile vile walikamata vifaa vya maabara, kemikali zinazoshukiwa kutumika kutengeneza dawa za kulevya.

Msako zaidi ulibaini shamba hilo limetumika kupalilia bangi na kuonyesha kuwepo shughuli haramu za mda mrefu.

Washukiwa wanatarajiwa kuwasilishwa mahakamani.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version