Sports
Manchester United Ndiyo mabingwa wa ‘PREMIERE LEAGUE SUMMER SERIES’
Manchester United imetwaa ubingwa wa kombe la ‘Premier League Summer Series’ kufuatia sare ya 2-2 dhidi ya Everton katika dimba la Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia Marekani.
Michuano hiyo ya maandalizi ya msimu mpya ilishirikisha timu nne za Ligi Kuu England Man United, West Ham United, Everton na Bournemouth ambapo Mashetani hao Wekundu wamemaliza kileleni pointi 7 baada ya mechi tatu, wakishinda mechi mbili na kutoka sare mechi moja.
Kiungo Bruno Fernandes aliwaweka uongozini United dakika ya 18 kupitia mkwaju wa Penalti au Tuta kisha Iliman Ndiaye akisawazishia The Toffees dakika ya 40,United tena walichukua uongozi kupitia kwa kiungo mshambulizi Mason Mount dakika ya 69 kabila ya beki Ayden Heaven kujifunga dakika ya 75.
MSIMAMO:
1. Man UTD — mechi 3 — pointi 7
2. West Ham mechi 3 — pointi 6
3. Bournemouth mechi 3 — pointi 3
4. Everton mechi 3 — pointi 1