Entertainment
Sijakataa Kuchangiwa, Ila Nipewe Heshima, Nyevu Fondo Afunguka
Muunda maudhui maarufu Pwani, Nyevu Fondo, amefunguka sababu zake za kukataa pesa za mchango wa matibabu zilizochangishwa na Presenter Jakki.
Presenter Jakki, bila kumjulisha Nyevu, alianzisha kampeni ya mchango wa matibabu kwa jina lake baada ya kujua Nyevu anaugua, akiwahamasisha mashabiki na wafuasi wake kutuma msaada wa fedha akishiriki picha za Nyevu Fondo kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza hewani kwenye kipindi cha Janjaruka 254, Nyevu alisema wazi kuwa hana tatizo na watu kumchangia, lakini alikerwa na jinsi jambo hilo lilivyofanywa bila ushauriano:
“Mimi sijakataa kuchangiwa. Ni kitu poa. Kitu ambacho kinaniumiza ni kuwa kwa nini hakuniuliza mimi mwenyewe, naugua nini na nahitaji msaada aina gani? Je, ule ugonjwa unahitaji msaada wa aina gani ama kile kitu nachougua kinahitaji msaada ama ala?”
Awali kwenye ukurasa wake wa Facebook Nyevu Fondo aliandika;
Hata hivyo Presenter Jakki hajanyamaza. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Jakki amejibu kwa hisia nzito, akieleza kusikitishwa na jinsi nia yake njema ilivyotafsiriwa vibaya mbele ya umma.
Hapa chini ni kauli yake kamili:
“Binadamu mbona tuna roho nyepesi kama korosho? 😢 Kwa nini mnanitengenezea taswira mbaya mbele ya hadhira yangu, ilhali nia yangu ilikuwa njema? Sitaki sifa wala umaarufu—nilitaka kusaidia kwa moyo wa huruma. Kumbukeni, kuna leo na kesho… na mitandao haitasahau kamwe. INTERNET NEVER FORGETS.”
“Kwa kuwa Nyevu Fondo hajaweza kupokea mchango huu, nimeamua pesa hizi nizielekeze kwenye kituo cha watoto yatima (Children’s Home) zikawe baraka kwa wengine. Labda Mungu ataniona na kunibariki. Kwa yote, nawaombea baraka – watu wa Mungu tuchukuliane kwa upendo.”
Awali Nyevu aliandika