News

Wanaharakati wanaitaka serikali kuifanyia marekebisho sheria ya dhamana

Published

on

Wadau wa kupambana na dhulma za kijinsia mjini Malindi kaunti ya Kilifi wameitaka serikali ya kitaifa kuifanyia marekebisho sheria ya adhabu na dhamana inayopewa washukiwa wa vitendo vya dhulma za kijinsia Mahakamani.

Wakiongozwa na James Chapa, wadau hao walisema hatua hiyo itasaidia pakubwa kukabiliana na visa vya dhulma za kijinsia pamoja na kuwazuia washukiwa wa visa hivyo kutohitilafiana na kesi hizo.

Chapa alisema sheria za sasa hazina makali ya kutosha ya kukabiliana na washukiwa wa visa vya dhulma za kijinsia hivyo basi kutatiza juhudi za kukomesha visa hivyo nchini hususan katika kaunti ya Kilifi.

“Ni lazima sheria zilizopo zifanyiwe marekebisho kwani hazina makali ya kukabiliana na dhulma za kijinsia ndio maana kuna shida katika kupata haki”, alisema Chapa.

Kauli yake imeungwa mkono na Afisa mkuu wa Idara ya jinsia kaunti ya Kilifi Goergina Abdul ambaye alitoa changamoto kwa serikali kubuni mikakati ya kuboresha utendakazi wa sheria hizo.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version