Sports
Kocha Wa Stars Benni McCarthy Atoa Sababu Ya Kujiondoa CECAFA
Mkufunzi wa Timu ya Taifa ya Soka Harambee Stars Benni McCarthy amesema kwamba walienda Tanzania kushiriki Kombe la CECAFA wakiwa na azma na ari kubwa ya kuhahakisha wanajiandaa vyema kwa taji la Chan mwezi Ujao ila mandhari waliokutana nayo hayakua ya kuridhisha ndipo wakafikia makubaliano ya kurejea nchini.
Akizungumza kwa mara ya kwanza vijana wa nyumbani wakizidi kujinoa Ugani Nyayo mwalimu huyo amekiri mortisha iliku juu mno ila mazingira hayo hayangeruhusu wao kufanya Kazi na kujianda Ugani Karatu Arusha. “Tuliketi chini kama benchi la Kiufundi tukaona ubora wa viwanja vya mazoezi na wa michezo tukaona itakua si salama kwa wachezaji kuelekea CHAN hivyo tukarejea”.
Haya yanajiri baada ya stars kujiondoa kwenye kipute Cha CECAFA Cha Mataifa Manne nchini Tanzania siku ya Jumatatu huku maswali chungu nzima yakibaki vinywani mwa wengi.
Hata hivyo mwalimu huyo anasema kwa sasa wanajitayarisha zaidi kwa Kombe Hilo kwani wanajua fika ugumu wa kundi lao.
Stars wako KUNDI A pamoja na Angola, Morocco, Zambia na DR.Congo.