News
Mombasa inaongoza kwa maambukizi ya TB
Kaunti ya Mombasa imetajwa miongoni mwa kaunti zinazoongoza kwa maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu eneo la pwani.
Everlyn Kibuchi mkurugenzi wa mradi wa kuhamasisha kuhusu ungojwa wa kifua kikuu unaofahakima kama Stop TB Project, alitaja mikusanyiko ya watu, ukosefu wa lishe bora na magonjwa ya kuambukiza miongoni mwa vinavyochangia maambukizi ya TB.
Akizungumza katika warsha iliyowaleta pamoja wanahabari jijini Mombasa, Kibuchi alisistiza umuhimu kwa jamii kufahamu dalili za maradhi ya kifua kikuu na kupata matibabu kwa wakati unaofaa.
“Mombasa ni eneo moja ambalo liko na janga kubwa sana la kifua kikuu nchini, changamoto ambayo inafanya kifua kikuu iwe shida zaidi hapa Mombasa ama pwani nimkwamba Tb inaenea zaidi mahali ambapo kuna mkusanyiko wa watu, kama mtu amepatikana na huo ugonjwa inafaa wale ambao wanaishi nayeye wao pia wanafaa wapimwe kwa sababu kunauwekano kuwa wameambukizwa”, alisema Kibuchi.
Mkurugeniz huyo vile vile alisema unyanyapaa miongoni mwa wanaoishi na ugonjwa wa kifua kikuu umechangia wengi kukosa kufanyiwa vipimo kwa hofu ya kupatikana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi.
“Watu wanaogopa kwenda kupimwa kwa sababu wakoishi katika hali ya unyayapaa, wanmajishuku pengine wakipatikana na kifua kikuu watapatikana na maambukizi ya ukimwi, sio watu watote ambao wako na kifua kikuu wanaishi na ukimwi, ni asilimia 23 ya watu Kenya nzima ambao wako na kifua kikuu na ambao wako na ukimwi, hii inamaanisha asilimia 70 hawana virusi”, aliongeza Kibuchi
Kwa upande wake Deche Sanga afisa anayesimamia kitengo cha ugonjwa wa kifua kikuu katika kaunti ya Kilifi, aliweka wazi kwamba waraibu wa dawa za kulevya 5,000 kaunti ya Kilifi wako katika hatari ya kuambukizwa maradhi ya TB, japo wameweka mikakati ya kukabiliana na hali hiyo.
“Kilifi tuko na takriban waru 5,000 wanaotumia dawa za kulevya, asimilia kubwa ya wanaoishi na TB wanaishi katika haya maeneo ambayo wanavuta unga, hii imefanya Kilifi tumekuja na mbinu ya kudhibiti hili tatizo, tumefungua vituo vya waraibu wa kurekebisha tabia tukishirikiana na wadau wengine, kwa mfano tuko na Omar project Malindi, malengo yake ni kupunguza madhara tukichanganya na HIV”, alisema Sanga.
Taarifa ya Joseph Jira