News

Wakaazi wa Malindi wanataka serikali kubuni mbinu za kuhifadhi miili ya Shakahola

Published

on

Wakaazi wa Malindi kaunti ya Kilifi walijitokeza na kuishinikiza serikali ya kitaifa kubuni mbinu mbadala za kuhifadhi miili ya watu iliyofukuliwa katika makaburi ya msitu wa Shakahola.

Wakaazi hao walisema kwa sasa wanalazimika kususia huduma za makafani ya hospitali kuu ya Malindi ambako miili hiyo inahifadhiwa hadi sasa.

Aidha walisema kwamba miili ya watu iliyofukuliwa Shakahola bado imelimbikizana kwenye makafani ya hospitali kuu ya Malindi bila ya hatua zozote madhubuti kuchukuliwa kuhusu miili hiyo.

“Tunashangaa jinsi serikali inavyoendesha shughuli zake hasa katika makafani ya hospitali kuu ya Malindi kwani ni zaidi ya miaka sasa bado kuna miili imesalia katika makafani hiyo

Wengi wa wakaazi wanasema kuwa inawagharimu kusaka huduma hizo kwenye hospitali za kibinafsi ambazo zinawatoza ada za juu mno.

Taarifa ya Hamis Kombe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version