Business
Wafanyibiashara Malindi Waelezea Kudorora Kwa Utalii Kutokana na Hoteli Kufungwa Eneo Hilo
Wafanyibiashara katika sekta ya utalii mjini Malindi kaunti ya Kilifi wameelezea kudorora kwa sekta hiyo kutokana na hatua ya mahoteli mengi eneo hilo kufungwa.
Wakizumguza na vyombo vya habari wafanyiabisha hao wakiongozwa na Boniface Mutuku, wamesema kuwa kufungwa kwa mahoteli kumewasababishia kukadiria hasara kwani kuna bidhaa nyingi ambazo hutumiwa na watalii sasa hivi zinaendelea kuharibika.
Kulingana hali hiyo imesababisha kupungua kwa kiwango kikubwa cha watalii ambao walikuwa wakizuru mji huo hapo awali hivyo kuathiri biashara zao.
Mutuku amemuomba gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Mung’aro kubuni mbinu za kufufua mahoteli yaliyosambaratika mjini Malindi ambayo yalikua kivutio kikubwa cha utalii eneo hilo ili kuboresha maisha yao.
Aidha ameongeza kuwa kupitia uboreshaji wa maeneo ya utalii na mahoteli nafasi za ajira zitaongezeka na kuboresha maisha ya wakaazi wa eneo hilo na kenya mzima kwa ujumla.
Kwa upande wake Anthony Muasya ambaye pia ni mmoja wa wafanyibiashara hao amewanyoshea kidole cha lawama baadhi ya viongozi mjini Malindi kwa kile anachodai kuwa wameshindwa kuwajibikia suala la kuboresha sekta ya utalii na pia viwanda.
Kulinanga na Muasya viongozi wako na uwezo wa kuboresha utalii na viwanda lakini kufikia sasa hakuna jambo lolote ambalo limefanyika kufikia sasa.
Amewataka viongozi hao kuwajibika ili kuhakikisha kuwa viwanda hivyo vinaimarika ili kuimarisha biashara zao.