News

Ndindi Nyoro:Serikali inakopa shilingi milioni 140 kwa saa

Published

on

Mbunge Kiharu Ndindi Nyoro amekosoa hatua ya serikali kutegemea mikopo inayozidi kuongezeka, kwa kutumia hazina za kitaifa kama dhamana kwa mipoko.

Nyoro alitaja hatua hiyo kama njia hatari ya kukopa ambayo inaweza kulemeza vizazi vijavyo.

Mbunge huyo alihoji mantiki ya kutumia ushuru wa mafuta na fedha za kurekebisha barabara kama dhamana ya kukopa hadi shilingi bilioni 100 kila mwezi.

Alisema hatua hiyo inakwepa kuangazia changamoto za msingi wa usimamizi wa umma akidai Kenya inakopa shilingi bilioni 3.4 kila siku sawa na shilingi milioni 140 kwa saa.

Aliongeza kuwa deni la kitaifa kwa sasa limefika zaidi ya shilingi trilioni 12.1.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version