Editor's Picks

Uamuzi wa Kesi dhidi ya kampuni ya Mayport Limited Wahairishwa

Published

on

Photo: Courtesy

Mahakama ya ardhi na mazingira katika kaunti ya Mombasa imeahirisha uamuzi wa kesi dhidi ya kampuni ya Mayport Limited inayohusishwa na mfanyabishara maarufu Mohamed Jaffar.

Mlalamishi katika kesi hiyo Juma Abdhallah Munyao amesema kampuni hiyo ilinyakua ardhi yake yenye thamani ya mamilioni ya pesa kinyume cha sheria.

Jaji Titus Naikuni, amesema amechukua hatua hiyo baada ya Wakili wa mlalamishi Steve Ogola kupitia kwa njia ya mtandao kueleza Mahakama kwamba alichelewa kuwasilisha majibu ya upande wa mlalamishi, akisema alikuwa mgonjwa.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo mwaka jana, Jaji Naikuni aliagiza kampuni ya Mayport Limited kupitia Wakili Shaniz Chatur na msaidizi wa Jaffar, Yakatali Amirali kuwasilisha hati miliki walizonazo kuthibitisha umiliki wa kipande hicho cha ardhi kinachozozaniwa.

Hata hivyo, wawili hao walishindwa mara kadhaa kuwasilisha stakabadhi hiyo mbele ya Mahakama pamoja na nyaraka zozote za malipo ya ununuzi wa ardhi hiyo huku walalamishi Juma Abdallah Munyao na Asma Nduku wakiwasilisha hati miliki halisi mbele ya Mahakama.

Hata hivyo Jaji Naikuni amesema pande zote mbili zitajulishwa tarehe ya uamuzi wa kesi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version