News
Nyanza yavuna Ksh 5.1B baada ya mkutano wa Rais Ruto na viongozi wa Nyanza, Ikulu
Rais William Ruto alikutana na kushauriana na viongozi kutoka eneo la Nyanza katika Ikulu ya Nairobi siku ya Alhamis.
Kulingana na taarifa kutoka Ikulu ya Nairobi, lengo kuu ya mkutano huo lilikiwa ni kutathmini maendeleo yaliyoafikiwa katika eneo la Nyanza.
Katika mkutano na viongozi hao kutoka eneo la Nyaza wakiongozwa na Gavana wa Siaya James Aggrey Orengo, Rais Ruto alisema kwamba serikali imetenga kima cha shilingi bilioni moja kwa ujenzi wa barabara ya Usenge kaunti ya Siaya.
Rais Ruto aliongeza kwamba, mradi huo ni miongoni mwa ile iliyoratibiwa kutekelezwa katika eneo la Nyanza na kutaja upanuzi wa Bandari za sehemu hiyo ili kuboresha biashara na sekta ya Uchumi wa bahari katika eneo hilo la Nyanza.
Katiak taarifa hiyo, Serikali pia itatumia kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kujenga masoko 16 na kiasi, shilingi bilioni 1.6 kufadhili mradi wa kuunganisha umeme kwa zaidi ya familia elfu 16.
Mkutano huu imefanyika siku mbili tu baada ya ziara ya Rais William Ruto katika kaunti ya Homabay ambako aliongoza taifa kuadhimisha sherehe za 62 Madaraka dei Juni, 1 2025.
Picha kwa hisani: Viongozi wa Pwani wakiwa na Rais Ruto Ikulu
Wachanganuzi wa masuala ya kiuchumi walisema ziara hiyo ni mafanikio makubwa kwa juhudi za viongozi wa Siaya, kinyume na ahadi zilizotolewa na serikali wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Ikulu na viongozi kutoka ukanda wa Pwani majuma macha yaliyopita.
Wakati wa mazungumzo hayo na viongozi wa Pwani, Rais Ruto aliahidi kujitolea kwa serikali kuboresha mazingira bora katika kukuza sekta ya Uchumi wa bahari kupitia mikakati ya maendeleo endelevu.
Mengine yaliyozungumzwa wakati wa mkutano huo ni pamoja na juhudi za serikali kumaliza tatizo la Uskwota katika ukanda wa Pwani na usimamizi wa Bandari ya Mombasa.
Mkutano huo ulikuwa umeoongozwa na Waziri wa madini na Uchumi wa bahari Hassan Ali Joho na mwenzake wa michezo Salim Mvurya.
Taarifa ya Eric Ponda