Sports
Noni Madueke Atua Arsenal
Sasa ni Rasmi Noni Madueke ni mali ya Arsenal vilabu vyote viwili vimekubaliana kwa ajili ya uhamisho huo wa pauni milioni 52 dhidi ya Muingereza huyo.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili mjini London kwa ajili ya vipimo vya kiafya kabila ya kumwaga wino mkataba wa miaka mitano na wanabunduki hao wa London Kaskazini.
Madueke mwenye umri wa miaka 23 anakua sajili wa nne kwa kocha Mikel Arteta baada ya kuwasili kwa kipa Kepa Arrizabalaga, kiungo wa Real Sociadad Martin Zubimendi na kiungo Christian Norgaard kutoka Brenford.
Nyota huyo amekua na kilabu ya The Blues nchini Marekani kwa kombe la Dunia baina ya vilabu huku akiacha kilabu yake ikijianda kwa fainali Jumapili hii.