News

Mwalimu wa Madrasa adaiwa kumlawiti mvulana eneo la Kwa Mwango mjini Kilifi

Published

on

Hali ya wasiwasi na ghasia zilishuhudiwa katika eneo la Kwa Mwango karibu na Mkoroshoni mjini Kilifi Agosti 28, 2025.

Hii ni baada ya wakaazi wenye hasira kuvamia madrassa ya msikiti wa Masjid Rehema, wakipinga tuhuma za udhalilishaji wa watoto unaofanywa na Mwalimu wa Madrasa hiyo.

Kulingana na walioshuhudia tukio hilo walisema kisa hicho kilidhiirika wakati mama mmoja alipofichua kwamba mwanawe ambaye ni mwanafunzi wa madrasa hiyo kwamba alilawitiwa na mwalimu mmoja wa madrasa hiyo.

Mama huyo ambaye alikuwa akipiga nduru na kulalamikia madhila aliyofanyiwa mwanawe yalisababisha umati wa watu kuvamia madrassa hiyo na bweni la wanafunzi hao, wakitaka kuchoma majengo ya madrassa hiyo kwenye msikiti huyo wa Masjid Rehema.

Wakaazi hao walivamia msikiti huo wakiwa na dhamira ya kumuadhibu Mhubiri huyo huku wengine wakifunga barabara ya Kilifi – Malindi pamoja na kuwasha moto, hali iliyosababisha msingamano wa magari katika eneo hilo ambalo kwa kawaida huwa na shughuli nyingi.

Wenyeji hao walivunja lango na kuingia msikitini na kuanza kumshanbulia Mhubiri huyo ambaya baadaye aliokolewa na Maafisa wa usalama ambao walimkamata mshukiwa na kumpeleka kituo cha Polisi mjini Kilifi.

Maafisa wa Polisi wamnusuru Mwalimu wa madrassa ya msikiti wa Masjid Rehema

Maafisa hao wa usalama wameeleza vyanzo vya habari Kwamba wanaendelea na Uchunguzi na mshukiwa atafikishwa mahakani hivi karibuni.

Taarofa ya Eric Ponda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version