Sports
Kikosi Cha Raga Morans Wamemaliza Ya Nne Mauritius
Kikosi cha Raga wachezaji saba kila upande chipukizi Morans kimemaliza nafasi ya nne mashindano ya Bara la Afrika nchini Mauritius.
Hii ni baada ya vijana hao kupoteza fainali ya kusaka nafasi ya tatu kwa alama 21-19 dhidi ya Zimbabwe jana jioni.Mechi hiyo ilianza kwa moto vijana wa nyumbani wakichukua uongozi wa mapema 10-0 na badaye 12-0 ila Zimbabwe wakarejea kwa moto wa radi na kuzamisha matumaini ya vijana hao kumaliza tatu bora.
Vijana hao waliwazidi nguvu Nigeria alama 43-12 katika mechi ya robo fainali kabila ya kupoteza 14-12 dhidi ya Madagascar katika mechi ya nusu fainali.
Blitboks ya Afrika Kusini ndiyo waliibukia na ushindi wakitandika Madagascar alama 28-12 katika fainali iliopigwa Jumapili na sasa timu hizo mbili zinakwenda kuwakilisha Bara Afrika katika mashindano ya dunia.