News
Kanisa Katoliki nchini lashinikiza maridhiano.
Kanisa Katoliki nchini limeshinikiza serikali na vijana kuridhiana ili kuepuka vurugu zaidi zinazoshuhudiwa nchini.
Askofu mkuu wa kanisa katoliki Athony Muheria wa Nyeri na Phillip Anyolo wa Dayosisi ya Nairobi, waliitaka serikali kuhakikisha wanaoathirika kwenye Dhulma za maandamano wanafidiwa.
Viongozi hao wa dini walisema kunaumuhimu wa kuthamini maisha ya binadamu na kushinikiza viongozi wa siasa kuepuka kutoa semi za kuchukiza upande wowote Ule.
Matamshi ya viongozi hao yalijiri wakati vijana wa kizazi cha Gen Z, pamoja na mashirika ya kijamii wakiendelea na maandalizi ya maandamano ya kumbukumbu ya yaliyojiri juni tarehe 25 mwaka 2025, wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha.
Wakati wa maandamano hayo baadhi ya vijana waandamamanaji walipoteza maisha, wengine kuacha na majeraha na wengine kutekwa nyara na kupotezwa katika njia tatanishi
Taarifa ya Joseph Jira